Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA STAMICO KWA KULETA MITAMBO MIKUBWA YA KUZALISHA RAFiKI BRIQUTTES


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Dustan Kitandula (Mb) imefanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa Mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes katika kiwanda kidogo kilichopo Msasani Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika ziara hiyo Mhe. Kitandula ameipongeza STAMICO kwa kuagiza mitambo mikubwa miwili.

Aidha ameitaka STAMICO kufungamanisha uzalishaji mkaa huu na Taasisi zingine zinazohusika ili kuufanya uwe wa kimkakati katika kupambana na ukataji miti ili ziweze kuleta manufaa kwa watanzania, Mhe Kitandula amesema

STAMICO imekuwa ikifanya kazi kubwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali hususani Nishati Mbadala ya Rafiki hivyo kuonesha nia ya dhati katika ya kupambana na ukataji miti hivyo.

Ameitaka STAMICO kuwashirikisha wale ambao ni wazalishaji wa mkaa wa kawaida ili kuwafanya wawe sehemu ya miradi ya taifa naa kuepuka kuwaondolea vyanzo vyao vya mapato.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Elsa Kapinga ameishauri STAMICO kuutangaza nishati hii mpya kwa nguvu ili iweze kujulikana na watanzania tanzania nzima.

Naye, Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa(Mb) amesema amepokea maelekezo yote yaliyotolewa na Kamati ya Nishati na Madini na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi.

Pia ameipongeza STAMICO Mhe. Kiruswa ameipongeza kwa kuendelea kuboresha uzalishaji wa mkaa kwa kuleta mitambo mikubwa na kuiweka sehemu tofauti za kimkakati.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO Meja Jenerali (mstaafu)

Michael Isamuhyo ameishukuru Kamati kwa kufanya ziara hiyo na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo na mapendekezo yote yaliyotolewa.

Aidha amesema STAMICO inaendelea kuimarisha mradi wa Rafiki Briquettes ili uzidi kuleta tija kwa wananchi.

Amesema hadi sasa STAMICO imeshaleta mitambo mikubwa miwili ambao imeshapelekwa mahali husika kwa ajili ya kusimikwa na kuanza uzalishaji

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imefanya ziara ya katika mradi wa Kuzalisha Mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes unaotekelezwa na STAMICO ili kuchangia jitihada za Serikali za kupunguza ukataji miti.