Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

MKURUGENZI MTENDAJI STAMICO AWATOA HOFU WAZILISHAJI WA CHUMVI MTWARA


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse ameshiri katika kikao cha Wadau wa Chumvi Mtwara, ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano Ofisi za Mkuu wa Mkoa Mtwara.

Akizungumza katika kikao kazi hicho cha kujadili Mikakati ya kuongeza idadi ya kaya zinazotumia madini joto, ameeleza kuwa Shirika limedhamiria kuongeza tija katika Sekta ya Chumvi kwa kusaidia ongezeko la viwanda vya uchakati chumvi nchini kupitia teknolojia itakayotumika kwenye kituo cha mfano kinachojengwa Kilwa mkoani Lindi. Kiwanda hicho cha kisasa kiko kwenye hatua za matengenezo nchini India.

Ameeleza kuwa kituo hicho kitakuwa mahsusi kwa ajili ya kuwasidia wazalishaji chumvi kupata elimu ya uzalishaji, kuongeza thamani chumvi na kupata soko endelevu la chumvi la wazalishaji wadogo wadogo.

Aidha amesisitiza kuwa kupitia teknolojia hiyo SIDO ina wakati mzuri wa kuchukua teknolojia hiyo na kutengeneza viwanda vidogo vidogo vya uchakataji chumvi vyenye tija kwa wazalishaji nchini.

Kupitia kikao hicho, Dkt. Mwasse amewapongeza Wazalishaji chumvi kwa kuwa wazi katika changamoto zao na kuahidi kutoa dira ya utekelezaji wa mradi wa kiwanda cha chumvi kwa kuweka Standard Operating Procedure (SOP) shirikishi ili kuleta tija kwa kiwanda kinachojengwa Kilwa.