News
MKURUGENZI MTENDAJI WA STAMICO AFURAHISHWA NA UTENDAJI WA WAFANYAKAZI WA MRADI WA UCHORONGAJI SHANTA - BUHEMBA
▪️Ahimiza wafanyakazi kufanya kazi kwa kujituma
▪️Aahidi kuendelea kuboresha maslahi ya Wafanyakazi kwa kadri uzalishaji utakavyoendelea kuwa mzuri.
▪️DHRA asisitiza uwajibikaji na kuwasihi wafanyakazi kuhakikisha mitambo inafanya kazi muda wote.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse leo tarehe 05 Agosti, 2025 ametembelea Mradi wa Uchorongaji wa Diamond Drilling (DD) wa Shanta Buhemba na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa kandarasi hii.
Katika ziara hii, Dkt Mwasse aliambatana na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bw. Deusdedith Magala, Msimamizi Mkuu wa Uchorongaji Bw. Alex Rutagwelela pamoja na Mha. Pili Athuman.
Dkt. Mwasse amejionea utekelezaji wa Kandarasi hii unaofanywa na Shirika kwa kutumia mitambo miwili ya Uchorongaji na kutoa pongezi kwa wafanyakazi na wasimamizi wa mradi kwa jitihada kubwa walizozifanya kuhakikisha kazi inaanza mara moja bila kusuasua.
Aidha, pamoja na pongezi hizo, Dkt. Mwasse amewataka wafanyakazi kuendelea kujituma na kuchapa kazi ili kuleta tija kwa Shirika na kuahidi kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kadri uzalishaji utakavyozidi kuwa mzuri.
Naye Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bw. Deusdedith Magala amesisitiza uwajibikaji kwa kila mfanyakazi na kuhakikisha kuwa mitambo inafanya kazi wakati wote ili Shirika liweze kupata faida na hatimae kulipa maslahi ya wafanyakazi.
Pia Msimamizi wa Uchorongaji Bw. Alex Rutagwelela amewahimiza wafanyakazi kufanya kazi kwa ufanisi huku wakizingatia usalama wa mitambo na afya za wafanyakazi ili kuepuka kusababisha ajali.
Kwa upande wao wafanyakazi,wameushukru uongozi wa Shirika kwa kutembelea mradi na kutoa hamasa ya kufanya kazi kwa bidii. Wafanyakazi hao wameahidi kuchapa kazi kwa weledi na kuhakikisha kuwa malengo ya Shirika yanafikiwa.
#MASTASHA