Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Madini

Shirika la Madini la Taifa

RAFIKI BRIQUETTES YA STAMICO RASMI KUTUMIKA CHUO CHA MAFUNZO ZANZIBAR

Imewekwa: 11 August, 2026
RAFIKI  BRIQUETTES YA STAMICO  RASMI KUTUMIKA  CHUO CHA MAFUNZO  ZANZIBAR

Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) katika muendelezo  wa kuhakikisha linaendelea kuwa kinara  katika kuhamasisha matumizi ya Nishati safi Tanzania nzima, leo tarehe 11/8/2026  limeingia mkataba  wa pande tatu na Chuo cha Mafunzo Zanzibar  na Taasisi ya Foundation for Disabilities Hope ( FDH )  ya kuhakikisha vyuo vyote  vya mafunzo ( Magereza) Zanzibar  vinaanza kutumia Nishati safi ya kupikia  ya Rafiki  Briquettes.

Makubaliano hayo yamefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar  na kushuhudiwa  na Kamishna  wa Magereza  Zanzibar Khamis Abdalah Khamis, Mkurugenzi  Mtendaji  wa STAMICO  Dkt. Venance  Mwasse na  Mkurugenzi  wa FDH  Bwn. Michael Salali.

Akiongea katika hafla hiyo, Dkt. Mwasse ameipongeza  Taasisi ya FDH kwa kufanikisha kuingia makubaliano  haya ambayo yatawezesha vyuo vyote vya Mafunzo (Magereza)  Zanzibar  kupata Nishati hii ya Rafiki Briquettes  ambayo  inaenda kuleta afueni kwenye  gharama za Nishati ya kupikia kwa vyuo hivyo  lakini pia kuanza kutekeleza agenda ya Nishati safi kwa Taasisi zote zinazohudumia watu zaidi ya 100.

Dkt. Mwasse  pia ameahidi kusaidia kuleta mafunzo na Kongamano  la  kuhamasisha  matumizi  ya Nishati safi   kwa Watumishi wa vyuo hivyo vya Mafunzo (Magereza) na Wananchi wote wa Zanzibar.

Awali akiongea na kutoa salamu kutoka FDH, Bwn. Salali ameahidi kushirikiana na  STAMICO  kuhakikisha Nishati hii inafika kwenye  vyuo vyote vya Mafunzo (Magereza) kwa wingi na inafika katika ubora unaostahili.

Naye, Kamishna Khamis ameishukuru na kuipongeza STAMICO  kwa kuhakikisha Nishati hii inafika  Zanzibar.

Ameomba pia STAMICO  iangalie namna ya kuwapa fursa hii  ya kusambaza  Nishati hii kwa wale  wafungwa ambao wamemaliza vifungo vyao ili iwe njia ya kujitengenezea kipato  baada ya kumaliza vifungo vyao.

Kamishna ameahidi kutoa ushirikiano  kwa STAMICO  na FDH katika  kuhakikisha  Nishati  hii inatumika katika Magereza  yote ya Zanzibar  kutekeleza agenda ya kuhakikisha taasisi zote zinazohudumia zaidi ya watu 100 zinatumia  Nishati safi katika matumizi yake ya kila siku.

STAMICO  imejipanga  kuhakikisha inaendelea  kuwa kinara katika kuhamasisha matumizi ya Nishati safi ya kupikia Tanzania nzima.

 

Mrejesho, Malalamiko au Wazo

slot gacor