Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO KUENDELEA KUWASHIKA MKONO WACHIMBAJI WA MADINI VIJANA NA WANAWAKE


*Dkt. Mwasse azidua duka la Madini ya Vito la Wachimbaji Vijana (Vijana Gem Shop)*

* ⁠*Vijana na Wanawake waoneshwa fursa katika uongezaji thamani madini*

Leo Ijumaa tarehe 12.07.2024 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse amezindua duka la madini ya Vito, *Vijana Gem Shop* duka lilipo Upanga, Dar es Salaam na linalomilikiwa na Chama cha Wachimbaji Wanawake (TAWOMA).

Hafla ya Uzinduzi umefanyika katika Ofisi ya TAWOMA, Jengo la STAMICO Mtaa wa Undali Jijini Dar es Salaam.

Katika Hotuba ya ufunguzi Dkt. Mwasse ameeleza uwepo wa fursa mbalimbali kwenye sekta ya Madini kuanzia kwenye uchimbaji hadi kwenye uongezaji thamani.

Ameongeza kuwa kupitia Malengo Endelevu (SDG) ambayo yanasisitiza Uwezeshaji Wanawake(*Women Empowerement*), Usawa wa Kijinsia (*Gender Equity*) na Maendeleo Endelevu (*Sustainable Development*) na Maendeleo Jumuishi (*Inclusive Development*) vijana na Wanawake wanayo fursa kubwa ya kunufaika na Rasilimali Madini kwa kushiriki kwenye shughuli za Uchimbaji na Uongezaji thamani.

Aidha, Dkt. Mwasse amewataka pia Taasisi za fedha (Mabenki) kuwezesha shughuli za uchimbaji na uongezaji thamani hususani madini ya vito na madini ya viwandani kwani sekta hii inakua kwa kasi na kuajiri watanzania wengi hususani Vijana na Wanawake.

Katika kuhitimisha hotuba yake

Dkt. Mwasse amesema STAMICO iko tayari kushirikiana na Wabia wa Maendeleo wakiwemo PACT Tanzania, Beutfull Story na MOYO Gem na Taasisi za nyingine za kifedha kuboresha na kuwezesha Wachimbaji Wadogo Vijana na Wanawake ili waweze kunufaika na rasimali Madini.

Kwa kufanya hivi tutakuwa tunaunga Mkono jitihada za Mhe. *Dkt Samia Suluhu Hasan* Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuongeza ajira nchini na kuwezesha sekta ya madini kuchangia vizuri kwenye Pato la Taifa, Alisema Dkt Mwasse.

Mkurugezi Mtendaji wa STAMICO amewapongeza TAWOMA - Youth kwa kuonesha mfano hususani kwenye shughuli za uongezaji thamani madini na Kufungua Duka la Madini (Vijana Gem Shop). Aidha ameupongeza uongozi wa TAWOMA chini ya Mwenyekiti wake Mama Semeni Malale (Iron lady) kwa ulipaji wa Kodi na Ada mbalimbali za Serikali na urudishaji faida kwa jamii (CSR).

Tukio hili la uzinduzi limehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo rais wa FEMATA Bw. John Bina, Mhe. Emanuel Silanga (M-NEC), RMO Mkoa wa Dar es Salaam, Wawakilishi kutoka PACT, Benki, Makampuni ya Madini, DACOREMA, Umoja Trust (Uganda), Chemba ya Migodi, Tanzania Youth in Mine (TYM),nk.