Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Madini la Taifa

STAMICO YATOA SOMO KATIKA KONGAMANO LA MADINI NA UWEKEZAJI ZAMBIA

Imewekwa: 26 October, 2026
STAMICO YATOA SOMO KATIKA KONGAMANO LA MADINI NA UWEKEZAJI ZAMBIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venence Bahati Mwasse, amezishauri nchi za Afrika kutumia wananchi wake na makampuni ya Serikali kuvuna rasilimali za nchi ikiwemo madini ili kukuza viwanda, ajira, uchumi na kuhakikisha uendelevu wa rasilimali hizo.

Ameyasema hayo Oktoba 23 2026 wakati akizungumza katika kongamano la madini na uwekezaji Zambia "Zambia Mining and Investment Forum 2026" lililoanza Oktoba 19 hadi 23 katika ukumbi wa MICC jijini Lusaka, Zambia na kubeba kauli mbiu isemayo "Transforming Africa's Mining Landscape".

Dkt. Mwasse alieleza kuwa ni vyema nchi ikashiriki uvunaji wa rasilimali zake kwa namna mbili kuu, yaani kwa kutumia watu wake yenyewe ama kutumia Taasisi ya Serikali ili kupata thamani stahiki ya kinachovunwa na kuwaletea maendeleo watu wake. 

Amesema, hii ni fursa ya kipekee ya wananchi kufurahia rasilimali walizonazo kwa kuwa rasilimali ni kwa ajili ya wananchi na ni jukumu la Serikali kuhakikisha wananchi wenye rasilimali hizo wananufaika ipasavyo na uvunaji makini na wa kisasa wa rasilimali unaongeza fursa za ajira, mapato na kuleta mageuzi ya viwanda katika nchi

Katika kusisitiza utendaji wa mashirika ya Serikali, Dkt. Mwasse ametolea mifano ya STAMICO na ZCCM-IH kama mashirika ya kuigwa na nchi nyingine katika uvunaji wa rasilimali za ndani.

"Njia bora ya kuhakikisha nchi inapata faida kubwa na stahiki kutokana na rasilimali zake ni kwa kuimarisha ushiriki wa kitaasisi katika uvunaji wa rasilimali hizo (state participation) kama ilivyofanya Tanzania na Zambia kupitia STAMICO na ZCCM-IH" alisema Dkt Mwasse.

Kwa kufanya hivyo nchi inatoa fursa ya mashirika kubeba ajenda za Serikali na kuyafanya mashirika kuwa lango la uingizaji wa mitaji ya kigeni nchini (FDI).

Naye, Mkurugenzi Msaidizi wa Uchimbaji Mkubwa wa Madini nchini Zambia Mha. Dalitso Mhango alisema ni muhimu sana kwa nchi ya Zambia kulitazama suala la uanzishwaji wa mfuko wa fedha kwa ajili ya wachimbaji wadogo (ASM Fund) kuwa eneo lenye umuhimu sana kwa kuwa kuna ongezeko kubwa la wachimbaji hao ambao wakiwezeshwa kifedha na utaalamu, nchi itazalisha mapato ya ndani kwa kiwango kikubwa zaidi na kusaidia kuondoa tatizo la ajira.

Kongamano hili lilifunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema Jumatatu ya tarehe 19 Oktoba, 2026.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo

slot gacor