Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Madini la Taifa

STAMICO KUENDELEZA LESENI ZA MADINI MKAKATI KWA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI

Imewekwa: 20 November, 2025
STAMICO KUENDELEZA LESENI ZA MADINI MKAKATI KWA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeingia Makubaliano (MOU) na Taasisi ya Utafiti na Uendelezaji Viwanda (TIRDO) lengo likiwa kufanya Utafiti wa madini ya Kimkakati (Strategic Minerals) nchini kwa lengo la kupata taarifa za uwepo wake na mashapo ili kuongeza uwekezaji kwenye madini haya na kuongeza manufaa ya kwenye uchumi wa nchi.

Makubaliano haya yameingiwa leo tarehe 11 Novemba 2025 Mkoani Morogoro baina ya Prof. Mkumbukwa Mtambo Mkurugenzi Mkuu -TIRDO na Dkt. Venance Mwasse Mkurugenzi Mtendaji-STAMICO. 

Akiongea umuhimu wa utafiti wa madini haya, Dkt. Mwasse alisema mashirikiano haya yanalenga kuongeza uwepo wa taarifa za mashapo ya madini mkakati zitakazosaidia uendelezaji wa madini haya kwa manufaa ya watanzania wote.

Aidha kwa upande wa TIRDO, Prof. Mtambo alieleza umuhimu wa mashirikiano haya kwani STAMICO Ina uzoefu na utaalam na vifaa vya utafiti kama mitambo ya uchorongaji ya kisasa yenye kuchimba zaidi ya mita 3,000 (3km).

Imeelezwa kuwa utafiti wa madini haya ya Kimkakati utawezesha kukuza sekta ya Viwanda nchini kwa kuvutia uwekezaji na hivyo kuongeza mchango wake kwenye Pato la Taifa.

Makubaliano haya yamehudhuriwa na Viongozi na Watalaam kutoka pande zote mbili wakiwemo; Mha. Ramson Mwilangali Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uhandisi-TIRDO, Mha. Baraka Manyama- Mkurugenzi wa Migodi na Huduma za Kihandisi-STAMICO na Bw. Fedrick Mangasini- Meneja Utafiti STAMICO 
 

Mrejesho, Malalamiko au Wazo