Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA WADAU MBALIMBALI


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini (STAMICO) Dkt Venance Mwasse ameahidi kuendeleza ushirikiano na wadau mbalimbali wa Shirika na wachimbaji wadogo. Hayo ameyasema wakati alipotembelea mabanda ya wadau wakati wa Maonesho ya Madini mkoani Geita Septemba 2023.

Awapongeza kwa kuendelea kutumia fursa ya Maonesho katika kuonesha kazi zao na kutoa elimu kwa wananchi hali unayoongeza uwazi na kupunguza migogoro baina yao na wananchi.

"Ni vyema tukatumia fursa hizi kutoa elimu ili kujenga uelewa kwa wananchi wajione nao ni shehemu ya miradi inayosimamiwa na Serikali."

Ametoa wito kwa Wachimbaji wadogo wanawake kuonesha kwa vitendo kazi wanazofanya za uchimbaji na zile za kuongeza thamani katika madini ili kuhamasisha wanawake wengine kuchangamkia fursa zilizomo katika sekta ya madini.

Amesema ni vyema wanawake wanaojishughulisha katika mnyororo mzima wa thamani wa madini kuungana na kuwa chini ya mwamvuli mmoja ili waweza kunufaika na misaada inayotolewa na wadau wa madini.

Akiongea kwa niaba ya wanawake wachimbaji katibu wa Chama cha Wanawake Wachimbaji ( TAWOMA) Bi Salma.. ameishukuru mlezi STAMICO kwa kuwaunganisha na taasisi za kifedha ambapo wameaanza kunufaika kwa kupata mikopo kapitia kwenye taasisi hizo.

STAMICO imekuwa ikifanya kazi na wawekezaji wenza, ambao ni Buckreef, Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu Mwanza, Kampuni tanzu ya STAMIGOLD sambamba na wachimbaji wadogo.