News
STAMICO YAFANYA MAKUBWA MKOANI GEITA
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) lapongezwa kwa kuanzisha na kuendeleza kampeni ya upandaji wa miti ya "STAMICO na Mazingira At 50" katika Mikoa mbalimbali nchi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko aliyekuwa mgeni rasmi katika zoezi la upandaji Miti na ugawaji wa vifaa vya Uchimbaji kwa wachimbaji wenye usikivu hafifu, lilofanyika Geita.
Mhe Biteko amesema Kampeni hiyo inayoenda sambamba na Kampeni ya usikate Miti hovyo tumia Mkaa Mbadala wa Rafiki Briquttea. Kupitia kampeni hii wananchi wana sisitizwa kutumia kutumia Mkaa Mbadala badala ya kutumia Kuni kwa kupikia.
Akizungumza kwenye tukio
hilo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini Mhe. Judith Kapinga ameelezea hali ilivyo kwa sasa ukataji miti ni wa kasi sana zaidi hekta laki nne za misitu upotea kila mwaka kutokana na ukataji wa miti unaosababishwa na shughuli mbali mbali hususani matumizi ya kuni na mkaa.
Mhe. Kapinga amesema hali ambayo inayosababisha kuwepo kwa athari kubwa za kimazingira na hapa Nchini kati ya hekari milioni moja inayokatwa asilimia 70 utumika katika uzalishaji wa mkaa hali ambayo inapelekea Nchi kuwa jangwa kwa asilimia 61.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt Venance Mwasse, amesema STAMICO itaendelea kusimamia kampeni yake ya kupanda miti sambamba na kuhudumia miti hiyo ili iweze kukua na kuleta tija katika mazingira.
Akiongelea vifaa vya uchimbaji amesema STAMICO imekuwa ikiwasaidia wachimbaji hao wenye usikivu hafifu ili kuhakikisha nao wanashiriki katika shughuli za kiuchumi za madini.
Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constantine Kanyasu ameipongeza STAMICO kwa juhudi hizi za kimazingira na kusema ni muda sasa wa Shirika hilo kuungana na wana Geita kurudisha uoto wa asili uliokuwepo zamani ili kupunguza majanga yanayoweza kutokea kutokana na kutoweka kwa misitu.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita,Cornel Magembe ameishukuru STAMICO na Wizara ya Madini kuendelea kuweka mikakati ya kutunza mazingira na kwamba Mkoa wa Geita hautarudi nyuma. Utaendelea kusimamia sheria za mazingira pamoja na misitu ili kuyatunza.
Akiongea wakati akitoa Salamu za shukrani Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo amewashukuru viongozi wote waliojumuika katika muendelezo wa Kampeni hii ya upandaji miti.
Na kuahidi kuungana bega kwa bega na viongozi wa Geita katika kuendeleza wachimbaji wadogo na kulinda mazingira kwa ujumla
Zoezi la upandaji miti limeenda sambamba na matembezi hisani pamoja na kugawa vifaa vya uchimbaji wadogo wenye usikivu hafifu.