Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YAFUNGUA MILANGO KWA WADAU WA KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA RAFIKI BRIQUETTES


Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) tarehe 20 Machi,2025 limekutana na kampuni ya ADC Tanzania kuandaa mkakati wa pamoja wa kuhamasisha wafanyabiashara na wajasiliamali wadogo kutumia nishati safi ya kupikia ya Rafiki Briquettes.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO CPA Dkt. Venance Mwasse wakati wa mkutano uliofanyika jijini Dar es Salam.

Kikao hiki ni hatua za awali za kuweka mikakati ya pamoja ya kuhamasisha matumizi ya nishati hii kwa wajasiliamali na wafanyabiashara wadogo wanaojishughulisha na sekta ya upishi wa chakula.

Amesema amefurahi kuona taasisi binafsi zinaweka dhamira ya kuchangia jitihada za Serikali za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Ameongeza kuwa ushirikiano huo utawezesha mambo matatu yakiwemo upatikanaji wa nishati safi, kurahisisha matumizi na kuhamasisha ufahamu na matumizi ya nishati hiyo.

Ameeleza namna STAMICO inavyojipambanua katika uzalishaji, usambazaji na uhamasishaji wa matumizi ya nishati hiyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ADC Tanzania, Bi. Ester Kitoka amesema kampuni yake imeanza kuangalia namna ya kuwawezesha wajasiliamali na wafanyabiashara wadogo na kati hususani kada ya chakula kuanza kutumia nishati safi yenye bei nafuu.

Amesema wamejipanga kuimarisha ushirika kati ya

mzalishaji na msambazaji sambamba na kuwajengea uwezo na kuwawezesha kutumia nishati safi