Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YAJIPANGA KUWA SHIRIKA LENYE MAUZO YA TRILLION


SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO), limesema kwa sasa sio tegemezi tena na lina mipango ya kwenda mbele zaidi ikiwa ni pamoja na kufanya uwekezaji mkubwa kimataifa.

Kauli hiyo ilitolewa Juni 24, 2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse, wakati wa kuzindua mitambo 10 ya uchorongaji na vifaa vya utafiti wa madini vyenye thamani ya Sh bilioni 12.41 kwa ajili ya shirika hilo, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Amesema kupitia mkakati huo uliowekwa, ifikapo mwaka 2030 litakuwa Shirika la madini la Daraja la Viwango vya Dunia (World Class State Mining Corporation) na kwamba litakuwa ni shirika lenye mauzo ya trilioni nyingi za fedha.

“Shirika la Madini tumeshaondoka kwenye utegemezi, tumeshaachana na kuwa kwenye Comfort Zone, tunaanza safari ya kuwa World Class State Mining Corporation ambayo kupitia andiko letu na slogan yetu ya MASTASHA (Make STAMICO Shine Again) tunakwenda kuwa Multi Trillion Turnover Corporation (Shirika la mauzo ya Trilioni nyingi) ifikapo 2030,” amesema Dr Venance Mwasse.