Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YATAKIWA KUZIDISHA UTOAJI WA ELIMU YA MATUMIZI YA MKAA MBADALA ZANZIBAR


Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amelipongeza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kupeleka Mkaa Mbadala Zanzibar na kuzitaka mamlaka husika kushirikiana na STAMICO ili kuhakikisha Mkaa unawafikia walengwa.


Hayo ameyasema Januari 9, 2023 alipotembelea banda la STAMICO katika ziara aliyoifanya kwenye Tamasha la Biashara linaloendelea kufanyika katika viwanja vya Maisara.


Ametoa pongezi kwa ubunifu wa mkaa na kuitaka STAMICO kundelea kutoa elimu kwa watu ili waweze kuelewa matumizi yake na kuweza kusaidia Utunzaji wa Mazingira.

Ameitaka STAMICO kushirikiana na Wizara, ofisi za Mikoa, Wilaya na Mamlaka husika ili kuweza kutoa elimu ya matumizi ya mkaa mbadala kwa ufasaa kwa wakazi wote wa Zanzibar.


Mhe. Abdula amesema "Tutakupeni kila aina ya ushirikiano, mshirikiane na Mamlaka zinazohusika Zanzibar ili muweze kutoa Taaluma hii, naamini jambo hili ni jema sana na litaweza kusaidia Zanzibar hasa katika kutunza mazingira.


Akiongea kwa upande wa STAMICO Meneja wa Masoko na Uhusiano Bw. Geofrey Meena ameshukuru kwa ukaribisho huo na kuahidi kuendeleza kampeni ya kutoa semina kwa watu ili kuhakikisha wanatumia mkaa mbadala ili kuokoa Mazingira.


Meena amesema sambamba na kushiriki katika Tamasha hili STAMICO inaendesha semina kwa watu mbalimbali katika willaya za Mkoa wa mjini ikiwemo wilaya ya mjini, magharibi A na magharibi B ambako mwitikio umekuwa mkubwa sana.


Kupitia agizo hili STAMICO inaenda kujipanga ili kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi wa Unguja na Pemba.


STAMICO imetumia Tamasha la Biashara Zanzibar kuleta hamasa ya matumizi ya mkaa mbadala wa kupikia wa Rafiki Briquettes ili kunusuru Miti inayokatwa kwa ajili ya nishati ya kupikia.