Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YAVUTIA WACHIMBAJI NA WAFANYABIASHARA KUUZA DHAHABU KATIKA KIWANDA CHA MWANZA PRECIOUS METALS REFINERY


Mnamo tarehe 14 Julai, 2023 Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kushirikiana na Mwanza Precious Metal Refinery (MPMR) limeitisha Kikao cha Wadau wa Biashara ya Madini ya dhahabu kutoka Mikoa ya Mwanza, Geita, Tabora, Mara na Kagera.

Wadau hawa ni Wafanyabiashara ya Madini ya dhahabu (Dealers), Wachimbaji Wadogo na wa Kati wa Madini na Brokers. Aidha kikao hicho kimeusisha Tume ya Madini na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Lengo la kikao hiki ilikuwa ni kujadiliana kuhusu fursa zilizopo kwa wadau wa madini kupitia kiwanda cha kisasa cha kusafisha dhahabu cha Mwanza Precious Metals Refinery (MPMR) kilichopo Mkoani Mwanza. Akieleza fursa zilizopo Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dr. Venance Mwasse amesema kupitia mabadiriko ya Sheria za kikodi kwa muuzaji wa dhahabu atakayeuza refinery, muuzaji atafaidika na *punguzo la mrabaha la 2%*, *ondoleo la ada ya ukaguzi (Inspection fee) asilimia moja (1%)*

Faida nyingine ni kuondolewa kwa kodi ya VAT kwa Mchimbaji wa Madini wa Kati na Mkubwa atayeuza dhahabu yake refinery.

Akifafanua zaidi, Bw. Deusdedith Magala, Mwenyekiti wa Kamati ya Uendeshaji wa pamoja (JMC) alisema Kiwanda cha Mwanza Refinery kinanunua dhahabu kutoka ndani na nje kwa bei shindani ya soko na kuisafisha kwa kiwango cha kimataifa 999.9 (purity) tayari kusafirishwa kwenda Soko la Kimataifa.

Kwa upande wao Tume ya Madini na TRA wamefafanua zaidi kuhusu vivutio hivyo vya kodi na kuwasihi wachimbaji wa dhahabu na dealers kuuza dhahabu zao kiwandani hapo.

Mara baada ya Kikao Wadau wa madini wameonesha utayari wa kuuza dhahabu zao Mwanza Refinery kwa kuwa ndio mkombozi wa biashara ya madini hapa nchini.

MPMR ni mradi wa ubia kati ya STAMICO na wawekezaji kutoka Dubai.