Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO yazindua kampeni ya STAMICO na Mazingira at 50 KWA KISHINDO


Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limezindua kampeni kupanda miti inayojulikana kwa jina la STAMICO na Mazingira At 50 ili kuhamasisha utunzaji wa Mazingira na kuunga mkono dhamira ya Serikali ya kuhifadhi mazingira.

Kampeni hii imezinduliwa katika mkutano wa Waandishi wa habari uliofanyika leo Agosti 2, 2022 jijini Dar es Salaam ikiwa ni moja ya shughuli itakayofanyika kuelekea maadhimisho ya Miaka 50 toka Shirika kuanzishwa kwa Shirika la Madini

Akiongea kuhusu kampeni hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse amesema kampeni hii imebeba kaulimbiu ya Panda Mti, tumia Mkaa Mbadala Rafiki Briquettes, okoa Mazingira na itazinduliwa tarehe 10 mwezi Agosti 2022 katika eneo la Ipagala jijini Dodoma" alisisitiza Dkt. Mwasse.

Amesema STAMICO inatarajia kupanda miti 10,000 ambapo kwa awamu ya kwanza itapandwa miti 100 katika jiji la Dodoma na baadaye katika maeneo mengine ambapo STAMICO inaendesha miradi yake.

Amesema, lengo ni kushiriki kikamilifu katika zoezi la kutunza uoto wa asili na kuleta hamasa ya kutunza mazingira ili shughuli za uchimbaji madini rafiki kwa mazingira.

Zoezi hili linafanyika kwa kushirikiana na Wizara ya Madini, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Ofisi ya Mkoa na Wilaya Dodoma, TAWOMA, TFS, na viongozi wa vikundi vya mazingira, vikundi vya wanawake katika mazingira.

Ametoa wito kwa watu wa Dodoma kushirikiana na STAMICO katika zoezi hili la upandaji miti.

Sambamba na kampeni hiyo STAMICO inatarajia kutoa vifaa kwa wachimbaji viziwi waliopo Nyakafuru Geita, na kutembelea Wagonjwa katika Taasisi ya Saratani Ocean road na kuzindua bidhaa ya Makaa mbadala Rafiki Briquettes ambayo itakapofika siku ya maadhimisho hayo.

Tanzania Census 2022