Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

TANZANIA YATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI AFRIKA KUSINI


Katibu Mkuu Wizara ya Madini Adolf Ndunguru ameongoza ujumbe wa Wizara hiyo na wadau wa madini kutoka Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Madini wa Indaba unaofanyika Jijini Cape Town nchini Afrika Kusini ambao unaenda sambamba na maonesho ya madini.

Mkutano huo ulianza Februari 6, 2023 jijini Cape Town na unatarajiwa kuhitimishwa Februari 9, 2023 ambao unashirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya Madini yakiwemo makampuni ya madini, watoa huduma katika Sekta ya Madini, Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi

Aidha, mkutano huo unatarajiwa kuwa na manufaa makubwa kwa nchi ya Tanzania ikiwemo kuhamasisha uwepo wa wawekezaji nchini kwa lengo la kuongeza tija kwenye uzalishaji wa madini na kukuza Pato la Taifa.

Pamoja na mambo mengine, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuyo ameipongeza Wizara ya Madini na Taasisi zake kwa kushiriki Mkutano huo.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Wizara ya Madini ameongozana na Kamishina wa Madini Dkt. Abdurahman Mwanga, na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt.Vanance Mwasse kufanya mazungumzo na wawikilishi wa makampuni ya Madini kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Marekani na Japan wakijadili kuhusu maendeleo ya Sekta ya Madini nchini hususan madini ya Kimkakati.