News
WASTAAFU WATOA FUNZO KWA WATUMISHI STAMICO
Watumishi wa Shirika la Madini laTaifa (STAMICO) wamekumbushwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kiutumishi wa umma ili kuweza kuleta tija kwa Shirika.
Hayo wamesemwa na Watumishi Bw. Geofrey Meena na Titus Saideya ambao wamestaafu na kuagwa leo Machi 13, 2025 katika ofisi za mkoa wa Dar es Salam.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wakitoa neno la shukrani Bw. Geofrey Meena aliyekuwa Meneja wa Masoko na Uhusiano STAMICO, amesisitiza umuhimu wa kujifunza kwa wengine, kufanya kazi kwa ubunifu na kushirikiana katika kuyafikia malengo ya Shirika.
Amesema STAMICO imekuwa sehemu nzuri ya kufanyakazi na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano pindi itakapohitajika.
Kwa upande wake Bw. Titus Saideya aliyekuwa Mkaguzi Mkuu STAMICO amezungumzia kuhusu kufanya kazi kwa kuzingatia haki kanuni na misingi bora ili kuepusha upendeleo na uonevu mahali pa kazi.
Amesema anaiona STAMICO
ikifika mbali kutokana na jitihada zinazofanya na viongozi katika kuhakisha Shirika linafikia malengo yake.
Amewakumbusha Watumishi wa STAMICO kushirikiana na viongozi na menejimenti ili kuweza kusonga mbele kiutendaji.
Kwa upande wa watumishi wanaobaki, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO bw.Deusidedith Magala amewashukuru Wastaafu hao kwa kuwa sehemu kubwa ya mafanikio ya Shirika kipindi chote ambacho walikuwa wakitumika Shirika hilo.
STAMICO imewaaga Watumishi wake wawili ambao wamestaafu kati ya Septemba 2024 …na Februari 2025.